Mbelgiji Simba Ashikiria Mkataba wa Niyonzima

Mbelgiji Simba Ashikiria Mkataba wa Niyonzima
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kwa sasa hajafikiria kumuachia kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima kutokana na uwezo alionao.

Aussems amesema kuwa wachezaji wengi waliopo Simba wana uwezo mkubwa hali ambayo inampa ugumu katika suala la upangaji wa namba ila ana uhakika wa kuwapa nafasi.

"Niyonzima ni mchezaji mzuri ana juhudi, hataondoka Simba kwa sasa, bado ana mkataba, kuhusu kupata namba hilo najua na ndio maana ninajitahidi kuhakikisha wachezaji wote wanapata namba kutokana na upana wa kikosi cha Simba," alisema.

Niyonzima anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Nyasa Big Bullets.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad