Mbunge Aliyekimbia Chadema Afunguka Kupewa Nafasi na CCM Kugombea Tena Ubunge Japo Wengi Wanakosoa

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Babati mjini kupitia Chama Cha Demoklrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadaye kutangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pauline Gekul, amesema hatua ya kurejeshwa kugombea nafasi hiyo si zawadi bali ni kitu alichostahili kwa kile alichokisema kuaminiwa na chama chake kipya.

Kada huyo mpya wa Chama Cha Mapinduzi, Pauline Gekul amesema hata kama watu wengi wanakosoa mimi kurudishiwa kuwania tena nafasi hiyo wana matatizo yao.

“Kwangu mimi kurudishiwa hii nafasi si zawadi bali nimepewa kazi na wamenipa wajibu wakufanya, kwa hiyo ni imani kubwa sana kwangu ambayo chama changu kimenipatia ya kuwania ubunge.”Amesema Gekul

“Na juzi nilifika ofisi ya mkurugenzi kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge muhimu tu naendelea kukishukuru chama changu kipya, na nitawawakilisha vizuri wananchi wakinichagua tena.”

Hivi karibuni Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi  iliwapitisha  Pauline Gekul kuwania Jimbo la Babati, James Milya jimbo la Simanjiro, Joseph Mkundi Jimbo la Ukerewe na Marwa Ryoba ambaye atawania nafasi ya ubunge jimbo la Serengeti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad