Kwa mujibu wa Mbunge huyo, aliamua kukaa kimya katika kipindi cha miaka mitatu ili kujua ni kwa jinsi gani serikali ya awamu ya tano inafanya kazi katika wizara ambayo yeye kama Waziiri Kivuli anaihudumia.
“Niliamua kutozungumza chochote kama Waziri kivuli wa Sera Bunge Kazi, Vijana na ajira kwa kipindi cha miaka 3 nione mwenendo wa serikali ya awamu ya tano inafanya nini, kuhusu wafanyakazi, vijana na bunge,” amesema Ester Bulaya.
“tuliwaambia dhamira ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa ni serikali kukwepa madeni inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo kwa sasa inafikia trilioni 8 kwa sababu waliwekeza kwenye miradi isiyokua na tija,” ameongeza.
Mbunge huyo alikuwa ni miongoni mwa wabunge ambao walikuwa wakitajwa huenda wakajiunga na Chama Cha Mapinduzi kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la waliokuwa wabunge wa upinzani kuhama vyama vyao kwa sababu mbalimbali ambapo kwa sasa ndiyo mara ya kwanza ameibuka na kuzungumza kwa umma.
|
kuwa wanaume ni wachoyo na wengine wanaogopa nguvu ya wanawake katika maendeleo.
Contact us