Mbunge Mwingine wa CUF Ajiuzulu Ubunge

Mbunge Mwingine wa CUF Ajiuzulu Ubunge
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Mtwara, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Katani Ahmadi Katani, leo Alhamisi Novemba 15,2018, amejiuzulu Ubunge na nafasi zake zote ndani ya chama chake.

Katani amesema kuwa kilichopelekea kujiuzulu nafasi hiyo na nyadhfa zake zote ndani ya CUF ni kutokana na chama chake kuwa na migogoro isiyokwisha, inayoathiri utendaji kazi wake.

Kupitia taarifa zilisombaa mitandaoni zimesomeka kuwa "Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Mtwara, kupitia Chama cha Wananchi CUF, Katani Ahmadi Katani, leo Alhamisi Novemba 15,2018, naye amejiuzulu Ubunge na nafasi zake zote ndani ya CUF, kutokana na chama chake kuwa na migogoro isiyokwisha, inayoathiri utendaji kazi wake".

Www.eatv.tv imemtafuta ili kutaka kufahamu kwa undani simu yake ya mkononi iliita bila mafanikio.

Katani anakuwa Mbunge wa kumi na moja kujiuzulu akitanguliwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea ambaye alitangaza kujivua nafasi yake ya ubunge kupitia Chama Cha Wananchi CUF, asubuhi bungeni leo kwa kile alichokieleza juu ya uwepo kwa mgogoro wa kiuongozi baina ya pande mbili za viongozi wa Chama hicho ikiwemo upande wa Lipumba na Maalim Seif.

Wabunge wengine ni Mwita Waitara (Ukonga), Julius Kalanga (Monduli), Chacha Marwa Ryoba (Serengeti),Godwin Moleli (Siha), James Ole Millya (Simanjiro), Pauline Gekul (Babati) na Joseph Mkundi (Ukerewe) huku upande wa CUF ni Maulid Mtulia (Kinondoni) na Zuberi Kachauka (Liwale .

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad