Mbunge wa CCM Amtaka Kocha was Taifa Stars Afukuzwe Kazi

Mbunge wa CCM Amtaka Kocha was Taifa Stars Afukuzwe Kazi
Mbunge wa Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuandaa barua ya kumfukuza kazi kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ili akishuka nchini akabidhiwe akitua tu uwanja wa ndege.

Lusinde (Kibajaji) ametoa kauli hiyo kufuatia matokeo ya jana ambapo Taifa Star ililala kwa bao 1-0 kutoka kwa Lesotho na kujiweka katika mazingira magumu ya kufuzu kwa Afcon 2019, Cameroon.

"Hii serikali mawaziri wanatumbuliwa wakikosea kidogo tu, sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache, namuomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje haraka mkataba," alisema Lusinde

Mbunge huyo alisema Kocha wa Taifa Stars, Amunike amekuwa na upendeleo wa upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi siyo kitaalum.

Kibajaji alisema sifa ya kocha wa Tanzania ni nidhamu kwa wachezaji ambayo watafundishwa jeshini, lakini suala la soka limemshinda.

Licha ya kuelezwa bado kuna tumaini la kusonga mbele, lakini Kibajaji alisema ndoto imeanza kufifia kwani timu ya Uganda iko vizuri wakati washindani wetu wanakutana na timu ambayo haiwezi kushindana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad