Mchungaji Ajitolea Kumaliza Matatizo ya Wema Afunga na Kumuombea

Mchungaji Ajitolea Kumaliza Matatizo ya Wema Afunga na Kumuombea
Mchungaji wa kanisa la Huduma ya Injili, Komando Mashimo amejitokesa na kusema yupo kwenye maombi ya kufunga akimwombea mwigizaji Wema Sepetu ili aipatwe na matatizo.

Wema Sepetu na Mchungaji Komando Mashimo

Mchungaji huyo amefunguka kupitia Friday Night Live ya East Africa Television ambapo amesema sababu kubwa ya yeye kufanya hivyo ni kwasababu Wema bado anahitajika kumtumikia Mungu ila jina lake limechezewa.

''Tumefanya maombi ya kwanza ambayo yalikuwa ni kukesha kwaajili ya toba lakini haya ya pili ni ya kufunga na kuomba kwaajili ya kusafisha jina lake ambalo limechafuliwa hivyo maaskofu na wachungaji wengine wafunge na kumwombea Wema'', amefunguka.

Mfungo huo wa maombi ulipangwa kufanyika Ijumaa ya Novemba 23, 2018, ambapo mchungaji Komando akiwa kama kinara wa wachungaji na manabii wa kanisa lake aliamuru wote nchini wafanye hivyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad