Mchungaji Msigwa aeleza sababu za mawakili wake kujitoa

Mchungaji Msigwa aeleza sababu za mawakili wake kujitoa
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema sababu ya mawakili wake kujitoa ni kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa kesi.

Ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 12, 2018 wakati akiiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam impe muda wa kutafuta wakili mwingine baada ya wakili aliyekuwa anamtetea Jamuhuri Jonson kujitoa.

Agosti 23, 2018 wakili Jeremiah Mtobesya alijitoa kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa kesi na Novenba 8, 2018 wakili Jamuhuri Jonson naye alijitoa kutokana na sababu hizo hizo.

Mchungaji Msigwa ameieleza Mahakama baada ya wakili wake kujitoa Novemba 8, 2018 kwamba muda ulikuwa mchache hivyo hakuweza kutafuta wakili na anaiomba Mahakama impe muda wa kutafuta wakili.

"Mawakili wangu wamekuwa wakijitoa kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa Mahakama jinsi inavyoendesha kesi zake.

"Naiomba Mahakama inipe muda wa kutosha ili niweze kutafuta wakili mzuri atakayeniwakilisha kutokana na uzito wa kesi.” Amedai Mchungaji Msigwa

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Wilbard Mashauri ametoa siku tano kwa Msigwa kuhakikisha anapata wakili wa kumtetea katika kesi hiyo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 23, mwaka huu.

Msigwa na viongozi wengine wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, wanashtakiwa kwa makosa tisa likiwamo la uchochezi na kuhamasisha mkusanyiko usio halali uliosababisha cha mwanafunzi Aqwilina
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad