Mchungaji Msigwa Azuiwa na Polisi Kufanya Mkutano

 Mchungaji Msigwa Azuiwa na Polisi Kufanya Mkutano
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Iringa kimesema mbunge wa chama hicho Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amezuiwa na polisi kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Iringa, Jackson Mnyawami amesema mkutano huo ulikuwa ufanyike leo, kwamba wamepokea barua ya polisi ikiwataka wasiendelee na mkutano huo.

Barua ya Novemba 21, 2018 iliyotolewa na mkuu wa polisi Wilaya ya Iringa kwenda kwa mbunge huyo inaeleza kuwa mkutano huo umezuiwa kutokana na taarifa za kiintelejensia.

“Polisi Iringa tunazo taarifa kuna kikundi cha watu wanaojiandaa kufanya fujo katika mkutano huo. Hali hiyo inaweza kuleta uvunjifu mkubwa wa amani,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

“Hakuna askari wa kutosha kwa ajili ya kusimamia mkutano huo kwani nguvu kazi kubwa imeelekezwa katika shughuli  maalum za kitaifa ya usimamizi wa mitihani ya kidato cha nne, cha pili na darasa la nne.”

Mnyawani amesema wameipokea barua hiyo ya polisi ikiwa na sababu mbalimbali.

“Sababu tulizoelezwa ni za kiintelejensia kwamba kuna watu watafanya vurugu lakini pia wamesema kuwa kuna shughuli za kitaifa, ikiwa ni pamoja na mitihani inayoendelea kufanywa na wanafunzi wa kidato cha nne,” amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad