Mganga wa Kienyeji adaiwa kumhadaa na kumbaka mwanamke wa miaka 20 aliyekwenda kupatiwa matibabu nyumbani kwake huko Muembe Majogoo wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja.
Akizungumza mwanamke huyo aliyedaiwa kufanyiwa kitendo hicho cha kiudhalilishaji amesema alikwenda kwa mganda huyo kwa lengo la kupatiwa matibabu lakini chakusikitisha Mganga alifunga mlango na kumtia karatasi yenye maandishi ya kiarabu katika sehemu zake za siri na kisha kumbaka jambo ambalo limemuweka katika wakati mgumu.
Sheha wa shehiya ya Muembe Majogoo Mwanahawa Haji Juma amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema “Tunavilaani vitendo hivyo lakini bado wapo wananchi wabaya wanaendelea kuvifanya, Serikali itamchukulia hatua muhusika aliyekifanya kitendo hicho”.
Wakizungumza baadhi ya majirani walioguswa na mkasa huo wamesema ni vyema wanawake wakawa makini wanapopewa masharti yasiyoeleweka na waganga wa kienyeji na wasikubali kuhadaiwa nao ili kuepuka kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa jamaa wa karibu wa Mwanamke wamesema teari wameshapeleka malalamiko yao kituo cha polisi Kijito Upele.