Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Babati mjini kupitia Chama Cha Demoklrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadaye kutangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pauline Gekul, amesema hatua ya kurejeshwa kugombea nafasi hiyo si zawadi bali ni kitu alichostahili kwa kile alichokisema kuaminiwa na chama chake kipya.
Akizungumza na www.eatv.tv kada huyo mpya wa Chama Cha Mapinduzi, Pauline Gekul amesema hata kama watu wengi wanakosoa mimi kurudishiwa kuwania tena nafasi hiyo wana matatizo yao.
“Kwangu mimi kurudishiwa hii nafasi si zawadi bali nimepewa kazi na wamenipa wajibu wakufanya, kwa hiyo ni imani kubwa sana kwangu ambayo chama changu kimenipatia ya kuwania ubunge.”Amesema Gekul
“Na juzi nilifika ofisi ya mkurugenzi kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge muhimu tu naendelea kukishukuru chama changu kipya, na nitawawakilisha vizuri wananchi wakinichagua tena.”
Hivi karibuni Chama cha Mapinduzi wabunge hao waliwapitisha jina la Pauline Gekul kuwania Jimbo la Babati, James Milya jimbo la Simanjiro, Joseph Mkundi Jimbo la Ukerewe na Marwa Ryoba ambaye atawania nafasi ya ubunge jimbo la Serengeti.
Aidha katika tamko hilo CCM kilitaja hadi tarehe 15 Novemba kuwa ndiyo tarehe ya mwisho kwa chama hicho kupokea maombi ya wenye nia ya kujiunga na chama hicho na kupewa dhamana ya uwakilishi kupitia tiketi ya CCM kwa wabunge na madiwani kutoka vyama vingine.