Akizung-umza na Showbiz Xtra, Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wa mkali wa Bongo Fleva, Vee Money alisema kwamba hajawahi kumtaja Rammy katika mahojiano yoyote kama anavyodai msanii huyo.
“Jamani hapana yule kaka nimemuona mara moja tu kwenye msiba wa Masogange alipozimia akiwa ameshika kitambaa na si vinginevyo kabisa, sijawahi wala kutamka sehemu kuwa nampenda au nataka kuonana naye,” alisema Mimi Mars.
Kwenye mahojiano ya gazeti dada la hili la Ijumaa, Rammy alisema anampenda sana Mimi na kudai kuwa anajua hata yeye anampenda kwani alishawahi kumsifia alipokuwa akihojiwa redio moja