Mjukuu wa Mangi Meli, amefanyiwa vipimo vya kinasaba vitakavyosaidia kusaka fuvu la chifu huyo aliyenyongwa na wakoloni wa Kijerumani mwaka 1900.
Mangi Meli alinyongwa baada ya kuongoza mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni na baadae kichwa chake kukatwa na kupelekwa Ujerumani.
Fuvu lake yawezekana kuwa ni moja kati ya mafuvu mengi yaliyopo kwenye makumbusho moja kubwa jijini Berlin.
Trump atetea mahusiano na Saudia, amezea mauaji ya Khashoggi
Sababu ya Tanzania kutumia wanajeshi msako Arusha
Wanaharakati wanataka fuvu hilo lirejeshwe ili lipate mazishi ya heshima anayostahili kama shujaa nyumbani kwao Moshi, kaskazini ya Tanzania.
Isaria Meli, mwenye miaka 87 ni mjukuu wa Chifu huyo wa jamii ya Wachaga amezitaka serikali za Tanzania na Ujerumani kushirikiana ili kuwezesha kupatikana na kurejeshwa kwa fuvu hilo.
Haki miliki ya pichaKONRADIN KUNZE
Image caption
Isaria Meli, 87, ni mjukuu wa Mangi Meli na anatamani kuona fuvu la babu yake likirudishwa.
Isaria alifanyiwa vipimo vya DNA jijini Berlin baada ya kukaribishwa na Wakfu wa Urithi wa Utamaduni wa Prussia (maarufu kama SPK) ambao unahifadhi mabaki ya mafuvu yalichukuliwa na wakoloni wa Kijerumani.
SPK tayari imeorodhesha mafuvu sita ambayo yanaaminika kutokea Moshi na yalihifadhiwa katika kipindi ambacho Chifu huyo aliuawa. Mafuvu yote hayo yameandikwa "Dschagga/Wadschagga" ikimaanisha Wachaga, ambalo ndilo kabila la Mangi Meli.
Watafiti wataangalia kama vinasaba vya DNA vya Isaria vitaendana na moja ya mafuvu hayo. Majibu yanatarajiwa kupatikana ndani ya miezi sita ya mwanzo ya mwaka ujao, 2019
Mjukuu wa Mangi Meli Afanyiwa DNA kutafuta Fuvu la Babu yake Mtemi wa Ujerumani
0
November 21, 2018
Tags