MWANAMITINDO maarufu nchini Hamisa Mobeto, ambaye pia mzazi mwenziye na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa angewaomba watu na mashabiki zake wamvumilie kwa muda yuko kwenye mahaba.
Akizungumza na Ijumaa, Hamisa alisema kuwa anajua watu wengi wangependa kumuoana anarudi nyumbani sasa hivi wajue ni kitu gani kinaendelea lakini amewaomba watulie kila kitu ambacho wananakitarajia kutoka kwake watakiona.
“Najua watu wengi mnataka kujua nikija nyumbani inakuwaje au mambo yangu yatakuaje mimi nimewaomba mtulie tuli mambo yataenda kama mnavyoniombea na yameshakuwa kabisa,” alisema Hamisa ambaye yuko kwenye ziara ya kimuziki nchini Marekani.