MNENGUAJI wa Diamond Platnumz, Moses Iyobo ‘Baba Cookie’ amfunguka kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani wakati wakielekea mkoani Mtwara kwenye Tamasha la Wasafi Festival 2018 lililofanyika Jumamosi katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani humo.
Akipiga stori na Global TV Online, Iyobo amesema wakiwa kwenye msafara wa zaidi ya magari 8 ya WCB na wasanii wenzao, alijikuta akidakwa na polisi baada ya kuvunja sheria za usalama barabarani kwa kuendesha gari kwa mwendokasi zaidi kuliko uliyoruhusiwa.
Mnenguaji huyo amedai baada ya kukamatwa alikuwa akibishana na askari na kushindwa kuelewana nao, ilisababisha awekwe ndani kwa takribani saa 9 kisha baadaye kuachiwa baada ya kulipa faini.
“Ujue tulikuwa tukiwahi kwenye shoo, tukitaka tufike haraka huku mzuka ukiwa mkubwa, kwa hiyo nilikuwa nakanyaga mafuta tu, sikufahamu kama eneo lile sikutakiwa kukimbia kwa spidi kubwa, walinikamata kutokana na kutoelewana nao wakanishikilia. Lakini baadaye waliniachia na shoo tulifanya vizuri.
Iyobo amesema kuwa hatorudia tena kuendesha kwa spidi kubwa na hata safari ya shoo yao ya Iringa itayaofanyika Ijumaa hii, atafata sheria, eneo la spidi kubwa ataendesha kama inavyotakiwa lakini eneo la spidi chini ya 50 atafuata sheria kikubwa wafike salama na kufanikisha Tamasha lao.
Akizungumzia maandalizi ya Shoo ya Iringa, Iyobo amesema wamejiandaa vizuri na watafamnya shoo kubwa zaidi kuliko ya Mtwara.
Mose Iyobo Afunguka Chanzo cha Kudakwa na Polisi Mtwara
0
November 28, 2018
Tags