Moto wateketeza mji wa 'Paradiso'

Moto wateketeza mji wa 'Paradiso'
Moto mkubwa unaoendelea kuwaka katika jiji la California nchini Marekani, umeteketeza majumba ya gharama kubwa yanayokaliwa na watu maarufu mbalimbali katika eneo la Malibu, ambako wenyewe wanauita mji wa Paradiso.


Moto huo ambao ulianza Alhamisi ya wiki hii, ulianzia msituni na kusambaa kwa zaidi ya heka 8,000, ambapo hata wataalamu wa kuzima moto nchini Marekani wameshindwa kuudhibiti.

Moja ya madhara makubwa yaliyosababishwa na moto huo ni vifo vya watu tisa mpaka sasa kamailivyoripotiwa na CNN, lakini pia kuteketeza majumba ya kifahari ya watu maarufu wa Hollywood zaidi ya 6,500, ikiwemo nyumba ya baba wa kambo wa kina Kim Kardashian na Caitlyn Jenner.

Masupastaa hao ambao wameingiwa na taharuki na kuyakimbia makazi yao wakiwa na watoto wa na 'pets' (wanyama wafugwao), huku wakitoa taarifa mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii juu ya usalama wao na madhara waliyoyapata.

Malibu ni eneo ambalo wasanii wengi wa Hollywood wanaishi, akiwemo Kanye West na mke wake KimKardshian, Khloe Kardashian, Lady Gaga, Will Smith na wengineo, na unaitwa 'City of Paradaise' kutokana na majumba hayo kuwa ya kifahari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad