Mpenzi wa Rayvanny Atoboa Siri ya Kudumu Kwenye Penzi Lao

Mpenzi was Rayvanny Atoboa Siri ya Kudumu Kwenye Penzi Lao
MZAZI mwenzake na msanii anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma ametaja siri inayomfanya kudumu na mpenzi wake huyo kwa muda mrefu.



Akipiga stori na Amani, Fahyma alisema kwamba, watu wengi huwa wanahisi yeye na mzazi mwenzake hawagombani kitu ambacho si kweli, huwa wanagombana mara nyingi ila upendo na uvumilivu ndivyo vinawafanya waendelee kudumu mpaka sasa.



“Kuna watu huwa wanafikiri mimi na mzazi mwenzangu hatugombani, kitu ambacho si kweli huwa tunagombana sana tu, ila sema binafsi nilishaamua kutulia naye, nampenda basi inatosha na ndiyo maana hamjawahi kusikia nina bwana mwingine zaidi yake,” alisema Fahyma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad