Mwimbaji Baraka the Prince amefunguka kuhusu Ruge Mutahaba ambapo ametumia ukurasa wake wa Instagram leo Nov 26, 2018 na kuandika mambo ambayo amedai kuwa hakuwahi kuyaongea popote kuhusu historia yake na Ruge ambayo ilianzia rasmi mwaka 2012.
Baraka ameandika haya…>>“Kitu ambacho sikuwai kukiongea popote katika history ya mziki wangu hapa nilipofikia ni UKUBWA wa MCHANGO wako katika music career yangu,Leo nitatoa story fupi kati yangu mi na wewe Boss wangu.Mnamo mwaka 2012 tarehe sina kumbu kumbu! Nilijaribu kukutafuta pasipo kujua ungerespond vipi jibu la shida yangu,Kutokana Ukubwa wako katika tasinia hii ya SANAA YA TANZANIA, na sikujua kama unaweza kuwa mtu wakujali alichonacho mtu yeyote pasipo kujali ni wa Adhi gani wala mnaukaribu gani Boss RUGE,na ukizingatia atukuwai kuwa na uhusiano wowote wakujuana kwa ukaribu ata umbali pia.
“Lakini uliweza kunipa nafasi na kuniambia nikutafute juma 3..Ilipo juma 3 nikakupigia unakipa kibali cha moja kwa moja kuja kuoanana na wewe #CMGmikocheni..Nilifurahi ajabu kwasababu nilijua ndoto yangu ya kwanza imetimia.Niliweza kufika office za #CLOUDSMEDIAGROUPCMG na nikaletwa moja kwa moja mpaka office kwako..Ulinipokea kwa UPENDO kama vile tuliwai kuonana hapo hawali..Ilinipa nguvu sana nakuona siku yangu special kwa hiyo siku,Uliweza kunisikiliza na kusikiliza baadhi ya nyimbo zangu na kuniambia mimi ni STAR mkubwa sana endapo kama nitajituma na kujitofautisha na mziki uliokuwa una trend kwa muda ule,Na akaniambia
“Nanukuu UNAUTOFAUTI MKUBWA NA WASANII WENGI KWENYE UPANDE WA SAUTI,LAKINI KUNA MTU UNAMKOPI (JINA NAIFADHI), ACHA KUIMBA KAMA HUYO ALAFU FANYA MZIKI WA WAKO PEKE YAKO, NITAFUTE ALHAMISI NIKUPE NYIMBO ZA KUSIKILIZA UTAJIFUNZA NA HAKIKA.. kisha ukanichukua na kunipeleka katika office za @suka5 na @tirarira2 na kunikabidhi kwako kisha ukawambia wanisikilize na kunisaidia kwa niaba yako..ITAENDELEA Get well soon #BONGOFLAVAFATHERRUGEMUTAHABA” – Baraka the Prince