Msanii Mrembo Pretty Kind Achekelea Kupata Blue Tick ya Instagram


MSANII wa filamu na muziki Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amejikuta akitoa ‘meno yote nje’ baada ya kutambulika kwenye Mtandao wa Instagram kwa kuwa na wafuasi wengi na kupata kitiki cha blue ambacho ni mastaa wachache wenye nacho.  Akistorisha na Risasi Jumamosi, Pretty alisema ana furaha kubwa kutambuliwa na mtandao huo kwani huko nyuma alikuwa akijisikia vibaya sana kuona wenzake wamewekewa, yeye hana.

“Kwa sasa nina furaha maana kwa kutambulika na mtandao nimejua kuwa nami ni staa, nilikuwa nawaonea donge sana wale ambao walikuwa wakiwekewa tiki ya kukubalika. Tiki hii imenipa nguvu zaidi ya kufanya kazi maana mtandaoni ni sehemu muhimu kutangazia kazi mpya,” alisema Pretty mwenye wafuasi 151,000.

STORI: Mwandishi Wetu, Dar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad