Stars itamkosa nahodha wake @samagoal77 katika mchezo wa kesho ambaye anatumikia adhabu ya kadi za njano, @msuva27 anasema, kukosekana kwake kunawapa morali na watapambana zaidi kwa lengo la kufuzu fainali za mataifa ya Afrika.
"Samatta ni mchezaji muhimu kwetu, mchezani ambaye anatupa sapoti kama wachezaji pia ni mzoefu. Tunamkosa lakini sisi wachezaji wenzake tumeweka nguvu na yeye ametuambia anaamini katika mechi hii tutafanya vizuri kwa sababu anaamini tutapambana"-Msuva.
"Tuko tayari kupambana kwenye mechi hii kwa sababu tunahitaji kufika hatua ambayo kila mtu anahitaji sisi tufike. Kila mchezaji anatamani kufika AFCON hilo ndio lengo letu kubwa."