MTANDAO wa Instagram jana Novemba 20 umetoa onyo kwa watumiaji wa mtandao huo ambao wanatumia Apps za kupata likes na followers feki kwenye akaunti zao kwani kwa sasa ujanja huo hautakuwepo tena kutokana na kuanzishwa kampeni ya kufuta likes na followers wote ambao ni bandia.
Sheria hiyo mpya ambayo imeanza kutumika tayari katika mtandao huo, itatumia mfumo wa mashine ambazo zitaondoa followers na likes zote feki, pamoja na komenti ambazo zimetoka nje ya mfumo wa kawaida wa mtandao huo.
Taarifa zinasema kwamba mtumiaji wa Instagram atapokea ujumbe wa kubadilisha neno la siri kwenye akaunti yake baada ya kupitiwa na kufutiwa likes na followers.
Mabadiliko hayo huenda yakawa tishio kwa akaunti ambazo zinafanya biashara ya matangazo kwenye mtandao huo, kwani wengi wamekuwa wakiwahadaa wateja wao kuwa kurasa zao zinatembelewa na watu wengi kwa kuwaonyesha likes, comments na followers wao na hata impression ya akaunti zao.
Hili ni tangazo kubwa la pili kutangazwa kwenye mtandao wa Instagram, baada ya mwanzoni mwa mwaka huu kutangaza kufuta akaunti zote feki kwenye mtandao huo.
Swala pia la Facebook kuwa polepole na kutokufanya kazi kwa wakati mwingine,wamesema pia watalifanyia kazi mapema.
Mtandao wa Instagram Watoa Onyo kwa Watumiaji Wake
0
November 21, 2018
Tags