Raia wa Tanzania amekamatwa akiwa ameficha mihadarati kwenye njia yake ya kwenda haja kubwa (rektamu).
Walikuwa safarini kuelekea China na India walipokamatwa Alhamisi usiku katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Mtanzania huyo ambaye ametambuliwa na idara ya uchunguzi wa jinai nchini Kenya kama Msafiri Musa alitoa tembe 47 za dawa za kulevya mara ya kwanza.
Aliwekwa chini ya uangalizi ambapo baadaye alitoa tembe nyingine 69. Polisi hawajasema raia wa mataifa hayo mengine ni kina nani.
"Wachunguzi wa jinai wamewasilisha maombi katika mahakama ya JKIA kumzuilia zaidi ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi. Washukiwa bado wanaendelea kuangaliwa kwa makini," idara ya uchunguzi wa jinai Kenya imesema kupitia ukurasa wake wa Twitter
Mtanzania akamatwa akiwa ameficha mihadarati njia ya kwenda haja kubwa uwanja wa JKIA Kenya
0
November 23, 2018
Tags