Adam Zakaria Kinyekire anajulikana zaidi kwa jina la 'Street Engineer', na yeye ni fundi mekanika kutoka Wilaya ya Tunduma, mkoa wa songwe, nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
Alijifunza kazi hiyo mwenyewe bila kuhudhuria chuo chochote, lakini ni maarufu kwa kuunda helikopta na pia huwafaa madereva kwa gereji lake la kuhama hama.
Adam anasema yeye ni mbunifu ambaye hakupata ujuzi wowote kutoka shuleni maana mara baada ya kumaliza shule ya msingi, alianza kujifunza kutengeneza magari katika karakana ya kawaida na baadaye akaanza kuunda vitu kama vile mashine ya kusagia nafaka, gari la karakana na hata helikopta.
"Ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali huwa sifundishwi na mtu ni kitu tu ambacho kipo kwenye damu, ni kama vile ndoto tu ambapo vitu vinakuja kwenye akili kwamba naweza kutengeneza hiki na hiki lakini sijawahi kupata mafunzo popote," Adam Zakaria anaeleza.
Mtaalamu wa nyoka aliyeandika safari ya kifo chake
Mtanzania achaguliwa katika wanawake bora 100 wa BBC 2018
Kwa sasa anafanya kazi na vijana takribani 40 na wengine zaidi ya 500 walipita katika mikono yake kupata mafunzo.
Kwa nini Adam aliamua kutengeneza gereji linaloweza kusafiri?
Sababu iliyompelekea kutengeneza gari la aina hiyo ni baada ya kubaini kwamba kuna wakati watu wanakosa huduma wakiwa mbali ndio maana akaamua kutengeneza mashine ambayo inatembea.
"Watu wengi huwa wanaharibikiwa na magari yao katika maeneo ambayo hakuna msaada."
Gari hili lina vitendea kazi vyote vya ufundi, mfumo wa umeme na huduma ya kwanza yaani kila kitu kinachopatikana kwenye garage kipo katika gari hili.
Wateja wangu wengi ni Watanzania ambao wana magari makubwa ya mizigo yanayoelekea au yanayotoka Zambia.
Zambia ina pori kubwa hivyo wakikwama inawawia vigumu kutengeneza.
Kampuni inayounda viatu vya ngozi ya kiboko na mbuni
"Kila siku magari yanakatika hivyo unaweza kukuta naenda mara mbili kwa wiki au mara nne kwa mwezi ila lazima niende", Adam aeleza.
Gari hili ambalo hulitumia kama gereji la kuhama hama, alilitengeneza kwa muda wa mwaka mmoja na sasa liko barabarani ni miaka saba, na anasema gari hilo lina manufaa makubwa sana sio kwake tu bali hata vijana ambao wanafanya nao kazi.
"Hii mashine inajitengeneza yenyewe na tunaweza kulipa ada za watoto shuleni," anasema Adam.
Hata hivyo bado anakabiliwa na changamoto ya kibali cha gari hilo ingawa anashukuru kuwa nchini Zambia huwa hawamsumbui kwa sababu limeunganishwa na gari jingine lenye namba ya usajili.
Gari linasafiri mpaka kilomita 600 kwenda kufuata magari yaliyoharibika nchini Zambia, mteja hulipa gharama ya huduma yake kulingana na kazi na eneo.
Mtanzania aliyetengeneza helikopta aunda gereji la kuhama hama linalohudumu hadi Zambia
0
November 20, 2018
Tags