Mtanzania Aliyetengeneza Herikopta Aunda Mtambo Mpya

Mtanzania Aliyetengeneza Herikopta Aunda Mtambo Mpya
Adam Zakaria Kinyekire anajulikana zaidi kwa jina la ‘Street Engineer’ na yeye ni fundi makenika kutoka Wilaya ya Tunduma, mkoa wa Songwe, Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania.



Alijifunza kazi hiyo  bila kuhudhuria chuo chochote, lakini ni maarufu kwa kuunda helikopta na pia huwafaa madereva kwa gereji lake la kuhamahama ambalo ni moja ya mwendelezo wa ubunifu wake.




Adam anasema yeye ni mbunifu ambaye hakupata ujuzi wowote kutoka shuleni maana mara baada ya kumaliza shule ya msingi, alianza kujifunza kutengeneza magari katika karakana ya kawaida na baadaye akaanza kuunda vitu kama vile mashine ya kusagia nafaka, gari la karakana na hata helikopta.



“Ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali huwa sifundishwi na mtu, ni kitu tu ambacho kipo kwenye damu, ni kama vile ndoto tu ambapo vitu vinakuja kwenye akili kwamba naweza kutengeneza hiki na hiki lakini sijawahi kupata mafunzo popote,” Adam Zakaria anaeleza.






Kwa sasa anafanya kazi na vijana takribani 40 na wengine zaidi ya 500 walipita katika mikono yake kupata mafunzo.



Hata hivyo bado anakabiliwa na changamoto ya kibali cha gari hilo ingawa anashukuru kuwa nchini Zambia huwa hawamsumbui kwa sababu limeunganishwa na gari jingine lenye namba ya usajili.






Gari linasafiri mpaka kilomita 600 kwenda kufuata magari yaliyoharibika nchini Zambia ambapo mteja hulipa gharama ya huduma yake kulingana na kazi na eneo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad