Mtanzania Joyce Msuya Ateuliwa Kuongozi Shirika la UN
0
November 21, 2018
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa kuwa kaimu kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira, UNEP.
Bi Msuya amekuwa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ambalo lina makao makuu yake jijini Nairobi, Kenya.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amenukuliwa na vyombo vya habari vya kimataifa akisema Antonio Guterres amechukua hatua hiyo huku akiendelea kumtafuta mkuu wa kudumu wa UNEP.
Nani hawa wanaotaka kumtuza Mange Kimambi?
'Wanawake hutekeleza mchango muhimu vitani katika jeshi'
Mwandishi afunguka kilichomkimbiza Tanzania
Wadhifa wa kiongozi wa UNEP ulikuwa umebaki wazi baada ya kujiuzulu kwa Erik Solheim ambaye amekumbwa na kashfa kuhusu gharama yake ya matumizi katika safari.
Mswada wa ripoti ya ukaguzi wa fedha ambayo ilipatikana na gazeti la Uingereza la Guardian, na ambayo BBC imefanikiwa kuisoma, inaonyesha Solheim alitumia jumla ya $488,518 (£382,111) akisafiri siku 529 kati ya siku 668.
Alikuwa hayupo afisini kwa takriban asilimia 80 ya muda wake kazini.
Ripoti hiyo inasema gharama hiyo imetia doa sifa za UN kama shirika ambalo huangazia masuala ya uhifadhi wa mazingira na uendelevu.
Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image caption
Erik Solheim alikuwa mkurugenzi mtendaji wa UNEP
Hakukuwa na mtu yeyote wa kufuatilia au kuwajibika kuhusu safari za kiongozi huyo.
Solheim amesema anatumai hatua yake ya kujiuzulu italifaa shirika hilo, na Umoja wa Mataifa kwa jumla
Tags