Mwamba wa Afrika, Jemedari Rais Magufuli Alipotutoa na Anapotupeleka


Na Emmanuel J. Shilatu

Ni miaka 3 sasa tangu utawala wa Serikali ya awamu ya 5 unaoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli iingie madarakani. Ni vyema tufanye tathmini tuone Rais Magufuli alipotutoa na anapotupeleka Watanzania.

1. Rais Magufuli anatutoa kwenye usafiri wa treni wa enzi za kikoloni unaotumia muda mrefu njiani anatupeleka kwenye ujenzi wa usafiri wa treni wa kisasa kwa standard gauge unaotumia umeme na muda mchache njiani kusafirisha Watu wengi na mizigo mingi.

2. Anatutoa kwenye usafiri wa anga wa ndege uliokufa anatupeleka kwenye ufufuo wa shirika la ndege lenye ndege kwa kununua ndege mpya saba ikiwemo Dreamliner 787-8.

3. Ametutoa kwenye shirika la simu lililokufa ametupeleka kwenye ufufuo wa shirika la simu linaloleta ushindani mkubwa kwenye makampuni ya simu yaliyokuwapo kutokana na ubora wa huduma na wa gharama nafuu.

4. Ametutoa kwenye uchumi uliokuwa asilimia 5.1 hapo awali mpaka kutupeleka kwenye uchumi unaokuwa wa zaidi ya asilimia 7.2

5. Ametutoa kwenye mzigo wa kulipia elimu mpaka kutupeleka kwenye unafuu wa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

6. Amewatoa akina Mama Wajawazito kwenye mateso ya kujifungulia sakafuni ametupeleka kwenye faraja kwa akina Mama Wajawazito kujifungulia vitandani. Mjamzito mmoja, kitanda kimoja.

7. Ametutoa kwenye mateso ya kulanguliwa dawa na ukosefu wa dawa kwenye hospitali za Serikali ametupeleka kwenye upatikanaji wa madawa mahospitalini uliofikia kiwango cha upatikanaji cha asilimia 89, tena kwa bei nafuu.

8. Ametutoa kwenye usumbufu na mateso kwa Wamachinga na Mama Ntilie kusumbuliwa na Wagambo mpaka kutupeleka kwenye utulivu na amani ya kutosumbuliwa kwa Wamachinga na Mama Ntilie.

9. Ametutoa kwenye mfumo wa kuleana na kuchekeana dhidi ya wabadhilifu na wala rushwa na kutupeleka kwenye mfumo wa uwajibikaji wa kupelekwa mahakamani kwa wala rushwa na Mafisadi. Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na mwaka 2017 na pia ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

10. Ametutoa kwenye mateso ya Wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati na kukosa maabara. Leo hii ametupeleka kwenye hatua ya ukamilifu wa uondoshaji wa tatizo la madawati nchi nzima na maabara kwa baadhi ya shule.

11. Anatutoa kwenye uondoshaji wa tatizo la foleni jijini Dar na kutupeleka kwenye ujenzi wa barabara za juu (flyovers) za Tazara na Ubungo. Flyover ya Tazara imeshaanza kutumika.

12. Amewatoa Wanazuoni wa chuo kikuu cha UDSM kwenye mateso ya kupanga na leo hii amewapeleka kwenye makazi bora ya mabweni ya kisasa wanayolipia gharama za chini kabisa.

13. Ametutoa kwenye balaa la utendaji na uwajibikaji wa hovyo kwa Watumishi wa umma na ametupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha kuridhisha cha uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma.

14. Ametutoa kwenye utitiri wa kodi kwenye kilimo na kutupeleka kwenye ufutwaji wa kodi mbalimbali za kilimo na kukifanya kuwa chenye tija kwa Wakulima. Leo hii bei ya korosho imepanda kutoka Tsh. 800 kwa kilo mpaka kufikia Tsh. 4000 kwa kilo.

15. Ametutoa kwenye usiri mkubwa wa mikataba na taarifa za madini na kutupeleka kwenye uwazi taarifa na mikataba ya madini. Leo hii tunajivunia mafanikio ya gawio sawia la faida za madini na Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini.

16. Ametutoa kwenye tatizo zito na sugu la ajira na kutupeleka kwenye ongezeko la fursa za ajira kupitia kwenye viwanda zaidi ya 3000, kuwatimua wenye vyeti vyeki, miradi ya ujenzi ya bomba la mafuta, flyovers na reli ya kisasa ya standard gauge.

17. Ametutoa kwenye makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 kwa mwezi mpaka kufikia kwenye makusanyo ya Tsh. Trilioni 1.3 kwa mwezi. Hali hiyo imeimarisha uwezo wa Serikali kibajeti.

18. Ametutoa kwenye urasimu na umangimeza kwa viongozi na kutupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi wa Serikali. Leo hii hakuna usumbufu kumuona kiongozi na viongozi wengi wapo site palipo shida za Wananchi wakizitatua.

19. Ametutoa kwenye mfumo wa walio nacho kujiona Mungu mtu na kuleta ukandamizi ndani ya jamii na kutupelekea kwenye uondoaji wa tabaka la uonevu kwenye masuala ya ardhi na sheria.

20. Ametutoa kwenye mkwamo wa Serikali kuhama Dar es Salaam na kutupeleka kwenye hamisho la Serikali kuhamia Dodoma. Mpaka sasa Waziri Mkuu, Wizara na idara mbalimbali zimehamia Dodoma. Tukumbuke mpango wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwepo na kushindikana kufanyika toka enzi za utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza.

21. Rais Magufuli ametutoa kutoka Wanafunzi Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu 98,000 hadi kufikia Wanafunzi Wanufaika 120,000 kwa sasa.

22. Rais Magufuli ametutoa kwenye makusanyo ya mapato ya madini kutoka Tsh. Bilioni 194 hadi kufikia mapato ya Tsh. Bilioni 301

23. Rais Magufuli ameyasimamia na kuyaimarisha vyema Mashirika ya umma. Kutokana na usimamizi imara mashirika 43 yametoa jumla ya gawio la TZS Bilioni 736.36 kwa Serikali. Kati ya hayo yapo ambayo hayajawahi kutoa gawio lolote lile tangu Uhuru.

24. Rais Magufuli na Serikali yake wamesimamia vyema vita dhidi ya rushwa na ufisadi na kupelekea jumla ya Tsh. Bilioni 127.9 kuokolewa kutokana na matendo ya rushwa.

25. Rais Magufuli amepunguza rufaa za Wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi kutoka Wagonjwa 558 mwaka 2015 hadi kufikia rufaa za Wagonjwa 108 mwaka 2018. Hii yote imetokana na kuimarishwa kwa huduma ya matibabu ya kibingwa nchini kwa kuboresha miundombinu na kununua vifaa tiba vya kisasa.

26. Rais Magufuli ametutoa kwenye uwepo wa vituo afya vinavyofanya upasuaji toka 115 nchi nzima tangu tupate Uhuru hadi kufikia vituo vya afya 208 vyenye uwezo wa kufanya upasuaji.

*Shilatu E.J*
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad