Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kuchana Mwana FA amesema kuwa kukua kwa sanaa nchini sio lazima wasanii watunge nyimbo zenye maudhui machafu au video zenye muonekano mbaya kwenye jamii, bali ni kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata kanuni na sheria.
Mwana FA amefunguka hayo alipokuwa anaongelea sakata linalokamata headlines hivi sasa la Wimbo wa Rayvanny na Diamond kufungiwa kutokana na kudaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mwana FA alifunguka haya zaidi:
Mimi napenda kuwashauri wasanii kuwa wanapotoa kazi zao wahakikishe wanatoa nyimbo ambazo zitaburudisha Lakini pia zisivuke mipaka ya kuharibu jamii kwasababu ukuaji wa Sanaa sio lazima wasanii watukane kwenye nyimbo au wawe uchi kwenye video zao hapana tubadilike kuna njia nyingi sana zilizo kwenye maadili”.
Mwana FA amesema hayo jana Novemba 14, 2018 muda mfupi baada ya kutoka BASATA ambako alienda kuwaombea msamaha wasanii wa WCB, Diamond na Rayvanny kuhusu kufungiwa wimbo wao wa Mwanza
Mwanaume FA Awapiga Dongo WCB "Kukua Kwa Sanaa Haimaanishi Lazima Wasanii Waimbe Matusi, Tubadilike"
0
November 16, 2018
Tags