Mwandishi Phocus Ndayizera azuiliwa Rwanda na kudaiwa kujihusisha na ugaidi

Mwandishi Phocus Ndayizera azuiliwa Rwanda na kudaiwa kujihusisha na ugaidi
Mwandishi wa habari wa kujitegemea Phocus Ndayizera ameonyeshwa mbele ya vyombo vya habari na polisi wa upelelezi nchini Rwanda wiki moja baada yake kutoweka.

Msemaji wa idara ya polisi ya upelelezi nchini humo amesema kwamba mwandishi huyo anatuhumiwa makosa ya ugaidi.

Mhadhiri aliyetaka kufikisha ujumbe kwa Magufuli UDSM
Magufuli awasifu Wachina, misaada yao 'haina masharti'
Mwandishi huyo alifanyia kazi vyombo vya habari mbali mbali na mara kwa mara amekuwa akiripotia BBC Idhaa ya Kinyarwanda na Kirundi yeye amesema kwamba hajui kwa nini anazuiliwa.

Mwandishi wa BBC aliyeko Kigali, Yves Bucyana, amesema Phocus Ndayizera wakati alipoonekana mbele ya waandishi wa habari kwenye makao makuu ya idara ya polisi inayohusika na upelelezi alikuwa amevalishwa pingu na hali yake ilionesha alikuwa mchovu.

Image caption
Phocus Ndayizera akiwa amefungwa pingu
Mwandishi huyo alifahamika katika vyombo vya habari mbali mbali na mara kwa mara aliifanyia kazi BBC idhaa ya Kinyarwanda na Kirundi kama mwandishi wa kujitegemea.

Mara ya mwisho kwa Phocus Ndayizera kuendelea kuiripotia idhaa ya BBC ilikuwa mwezi wa Juni mwaka huu.


Alipotakiwa na polisi kuwambia waandishi wa habari tuhuma dhidi yake, Bwa Ndayizera amesema kwamba hana habari yoyote kuhusu mashitaka dhidi yake akisisitiza tu kwamba na yeye anasubiri upelelezi kukamilika.

Amesema kwamba alikamatwa katika mtaa wa Nyamirambo jijini Kigali alipokwenda kumuona jamaa yake na kupelekwa sehemu isiyojulikana kabla ya kujikuta katika mahabusu ya polisi kituo cha Remera.

Msemaji wa idara ya upelelezi Modeste Mbabazi amewambia waandishi wa habari kwamba Ndayizera anatuhumiwa kwa kujihusha na ugaidi
Polisi wa upelelezi wamekiri kuwa ndio waliokuwa wanamshikilia mwandishi huyo kwa wiki nzima.

Msemaji wa idara ya upelelezi Modeste Mbabazi amewambia waandishi wa habari kwamba Ndayizera anatuhumiwa kwa kujihusha na ugaidi na pia kukutwa na vifaa vya vilipuzi.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, walikuwa na taarifa za mipango ya watuhumiwa kutumia vilipuzi kuhatarisha usalama wa nchi ya Rwanda.

Msemaji wa Polisi amesema walisubiri siku kadhaa kutangaza kumshikilia mwandishi huyo kutokana na kwamba makosa ya ugaidi yanafwatiliwa kwa njia ya kipekee tofauti na makosa mengine.

Haijafahamika ni lini mwandishi huyo na wengine wanaotuhumiwa pamoja watakapofikishwa mahakamani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad