Kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya,Henery Mwaibambe aliwaambia waandishi wa habari kituoni hapo leo kuwa marehemu aligongwa na gari wakati akipata kinywaji cha kahawa akiwa na wenzake mjini hapo na kufariki dunia papo hapo.
Mwaibambe aliongeza kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva wake Salala Nyakiriga 67 mkazi wa Obwere ambapo aliogonga Mwenyekiti huyo wakati akijitahidi kuondoa gari lilipokuwa limepaki.
"Jeshi la polisi linamshikilia mmiliki wa gari aina ya Nadia lenye namba za usajili T 264 DLA kwa kosa la kumgonga mwenyekiti wa UWT Wilaya Rorya na kumsababishia kifo pamoja na mwenzake Veredian Otonya 50 makzi wa Obwere na kumjeruhi hali iliyosababisha kupelekwa hospitali kulazwa kwa lengo la kupatiwa matibabu"alisema Mwaibambe.
Mwaibambe aliwaambia waandishi wa habari kuwa tuki hilo lilitokea majira ya saa 1.15 jioni 12,2018 katika mji huo wakati dereva huyo alipokuwa amepaki gari yake kwa lengo la kupata kinywaji cha pombe aina ya bia ndipo alipoondoa gari na kusababisha kifo cha mama huyo.
Kamanda Mwaibambe ametaja chanzo cha kifo cha mwenyekiti huyo ni ulevi wa kupita kiasi ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka waendesha vyombo vya moto kuacha tabia ya ulevi wanapokuwa wakitumia vyombo vya moto.
Kamanda huyo pia ameongeza kuwa mwili wa marehemu umekabidhiwa ndugu zake baada ya uchunguzi wa polisi kwaajili ya mazishi na kuwa dereva huyo anahojiwa pindi upelelezi utakapo kamilika atafikishwa mahakamani kukabiliana na mkono wa sheria.
Kwa upande wa shuhuda wa tukio hilo Otieno Onyango alisema kuwa alishuhudia dereva huyo aliondosha gari kwa kurudi nyuma hadi walipokuwa wamekaa wakina mama hao wakipata kinywaji na kumgonga mwenyekiti na kufa papo hapo na kujeruhi mwengine hali ambayo ilizua tafaruku katika mji huo.