Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi Yanga Tanzania, Bakili Makele, amesema leo ataenda katika Shirikisho la Soka nchini (TFF) kueleza kwanini amepinga klabu hiyo kusimamiwa uchaguzi wake na shirikisho.
Kamati ya Maandili ya TFF imemuita Makele kwenda kueleza hoja za msingi za kupinga suala hilo baada ya kupewa maagizo na Baraza la Michezo Tanzania (BMT).
Makele amekuwa mmoja wa viongozi na wanachama Yanga wanaopinga maamuzi ya BMT kuitaka TFF isimamie uchaguzi wa klabu yao wakisema haina kamati inayojitosheleza.
Hata hivyo Makele amefunguka na kusema hajaona sababu ya msingi ya kuitwa TFF akieleza hoja walizompatia akajieleze hazina mashiko hivyo ataenda kutimiza wajibu.
Makele bado ameonekana kuwa na msimamo wa kuungana na wanachama wenzake kupinga kwa uzito juu ya TFF kutaka iisimamie Yanga uchaguzi wake ambao umepangwa kufanyika Januari 1 2019.