Nahreel Ataka Mashabiki Watengenezwe


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Mkono 'Nahreel' anaeunda kundi la Navy kenzo, amesema  vitu vya msingi katika muziki vipewe nafasi kubwa kama vile kiki zinavyo heshimika katika soko la muziki.

Akizungumza na www.eatv.tv, Nahreel amesema wasanii, vyombo vya habari pamoja na wadau wa muziki, hawazungumzii matukio muhimu katika muziki, kama vile msanii kutoa ablumu mpya au kufanya tamasha kubwa, kitu ambacho kinawafanya mashabiki wengine kuona havina umuhimu mkubwa kama vile matukio ya kiki.

''Ukubwa wa tukio katika soko la muziki hutengenezwa na msanii au vyombo vya habari, kwahiyo shabiki huamini katika msanii lakini pia chombo cha habari, na ngumu sana kumfanya afuatilie kitu ambacho hakizungumzwi'', amesema Nahreel.

Nahreel ameongeza kuwa vyombo vya habari na wasanii viwatengenezee mazingira mazuri mashabiki wa muziki ili wafuatilie mambo yakimaendeleo zaidi katika soko la muziki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad