Naibu Spika Awakaanga Wabunge wa Upinzani

Naibu Spika awakaanga wabunge wa upinzani
Naibu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amesema wabunge wengi wa upinzani huwa hawafuati taratibu pindi wanapotaka kuchangia michango yao kwenye bunge.

Kauli hiyo ya Naibu Spika ameitoa kufuatia kuwepo kwa malalamiko juu ya namna ambayo amekuwa akiwazuia wabunge wa upinzani kutoa michango yao ambapo amekuwa akiwazuia mara kwa mara.

“Jamii inapaswa kujua kuna wabunge wengi sana, ndio maana tumeweka kanuni na taratibu ili wabunge wazifuate wakati mwingine wapinzani hawazifuati, kwa hiyo kama kiti cha spika kazi yake ni kusimamia utaratibu tu, tatizo jingine jamii huwa inapenda kutafsiri upinzani unaonewa.” Amesema Naibu Spika

“Hakuna kuonewa kwenye bunge, mengi yanaamuliwa na bunge zima ila mambo machache ndio yanaamuliwa na kamati za bunge ambapo kuna wabunge wote wa upinzani.”

Aidha Naibu Spika huyo amesema atagombea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ikiwa ni mkakati wake wa kuhakikisha anaongeza idadi ya wabunge wanawake wa kuchaguliwa bungeni.

“Juhudi ninazozifanya nikikutana na wanawake wenzangu  huwa tunaaambiana sisi kama wabunge wanawake tunashauriana tuache ubunge wa viti maalum ili twende tukagombee kwenye majimbo.” Amesema Naibu Spika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad