Naibu Waziri wa Ujenzi anusurika kifo ajalini


Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye leo Jumapili Novemba 11, amenusurika kifo baada kupata ajali eneo la Iguguno Kata ya Mkalama mkoani Singida.


Naibu waziri huyo amesema alikuwa katika ziara ya kikazi lakini anamshukuru Mungu yeye na alioambatana nao katika msafara huo wametoka salama.


“Ni kweli tumepata ajali, ilikuwa kilomita 25 kabla ya kuingia Singida nilikuwa natokea Nzega kikazi lakini namshukuru Mungu tumetoka salama wote,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad