Naj Hakujua Kama Nabadilisha Dini- Barakah The Prince

Naj Hakujua Kama Nabadilisha Dini”- Barakah The Prince
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince ameibuka na kudai Mpenzi wake Naj hakuwa na taarifa kuwa amebadilisha dini.

Barakah amefunguka hayo Baada ya tetesi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Barakah amebadili dini kisa mpenzi wake Naj ambaye ni  Muislamu.


Katika mahojiano yake na mtandao wa Dizzim Online, Barakah ameweka wazi kuwa alipofikia uwamuzi wa kubadilisha dini hakumshirikisha mpenzi wake Naj mpaka zoezi lile lilipokamilika:

Ni kweli kabisa nimebadili dini kutoka ukristo na kuwa Muislamu na hivi sasa naitwa Abdulmalik na nilifanya kwa maamuzi yangu mwenyewe kwa sababu mimi sio wa kwanza, kuna ndugu zangu kibao kwenye familia yangu wamekwisha badilisha dini na Naj mwenyewe hakujua kama nimebadilisha dini mpaka alivyoona mtandaoni, nilimficha sikutaka ajue”.

Taarifa zilisambaa Kuwa huenda Barakah aliamua kubadilisha dini ili apate kufunga ndoa na mpenzi wake huyo ambaye anaishi majuu kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad