AKIULIZA swali bungeni jijini Dodoma leo, Jumatatu, Novemba 12, 2018, Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, ameitaka Serikali kutoa majibu ni wapi zitapatikana fedha za kuchangia elimu mkoani Lindi ikiwa korosho hazijauzwa na kusema yaliyotokea kwenye korosho yanajulikana.
“Mheshimiwa mwenyekiti, sisi mkoa wa Lindi tulikubaliana kukata shilingi 30 kwa kilo ya korosho ili kuchangia elimu na mwaka jana katika jimbo langu pekee zilipatikana zaidi Sh 400 milioni lakini yaliyotokea sote tunajua, je, nini mkakati wa serikali katika hilo?” amehoji Nape.
Akijibu swali, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Josephat Kandege, aliwambia Nape kwamba alitamani korosho zinunuliwe, lakini yale yaliyopangwa kwenye maendeleo lazima yaendelee huku mipango mingine iliyopo kuhusu zao hilo ikifanywa.