Ndege Yaupita Uwanja wa Ndege kwa Kilomita 50 Baada ya Rubani Kushikwa na Usingizi

Ndege Yaupita Uwanja wa Ndege kwa Kilomita 50 Baada ya Rubani Kushikwa na Usingizi
Ndege ndogo ilipita uwanja iliostahili kutua nchini Australia kwa karibu kilomita 50 baada ya rubani kushikwa na usingizi, kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa angani.

Rubani alikuwa peke yake kwenye ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Devonport kwenda King Island huko Tasmania tarehe 8 Novemba.

Kisa hicho kwa sasa kinachunguwa na mamlaka za usafiri nchini Astralia (ATSB).

Maafisa hawajasema jinsi rubani huyo alifanikiwa kuamka na kutua salama.

Wakati ikiwa angani rubani alilala hali iliyosababisha ndege hiyo kupita uwanja na kuendelea na safari kwa kilomita 46 zaidi.


Mtaalamu wa usafiri wa ndege Neil Hansford alisema Australia ina sheria kali zinazohusu uchovu wa rubani.

"Hakuna vile popote pale duniani mtu anaweza kuendesha ndege akiwa amechoka," alikiambia kituo cha habari ya serikali cha Australia.

Kwenye mtandao wake, Vortex Air inasema hufanya safari za ndege kwa vikundi, makampuni na safari za starehe kote nchini Australia.

ATSB ilisema itamfanyia mahojiano rubani na kuchunguza mipangilio ya huduma za shirika hilo kabla ya kutoa ripoti yake mwaka ujao.

Mwaka uliopita watu watano waliuawa wakati ndege iliyokuwa safarini kwenda King Island ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Melbourne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad