Ndugai Afunguka Kuhusu Kuwachongea Mawaziri kwa Rais Magufuli

Ndugai Afunguka Kuhusu Kuwachongea Mawaziri kwa Rais Magufuli
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema lengo la kuwataja Mawaziri na Wabunge ambao wana mahudhurio hafifu ndani ya Bunge haikuwa kuwachongea kwa viongozi wa vyama vyao bali ni kuwataka wabunge hao kutimiza wajibu wao wa kuingia bungeni.

Kwa mujibu wa Spika Ndugai Mawaziri wengi wanashindwa kuhudhuria bungeni, kwa kisingizio cha  kuwa wako kwenye maeneo mbalimbali wanatatua changamoto za wananchi wakati wawakilishi wao wako bungeni.

Akizungumza na www.eatv.tv Spika Ndugai amesema “nia haikuwa kumchongea mbunge yeyote, kumbuka hata mawaziri nao wanakuwa wabunge kabla ya kuwa mawaziri, na uzuri wa bunge letu linaratiba ya mwaka mzima, wanapokuja pale wanakuja na ratiba nchi nzima,
haiwezekani mimi mbunge wa Kongwa bunge linaendelea halafu Waziri anaenda Kongwa.”

“Kwa sasa siwezi kuwataja tena, orodha ya wabunge ambao ni watoro ila kwa faida ya wananchi tutawatajia mwishoni ili inapofika kipindi cha uchaguzi, watambue ni mbunge gani ambaye walimuagiza bungeni lakini alikuwa ahudhurii,” amesema.

“Mfano huyo Mbunge wa Arusha Mjini (Godbless Lema,) kutwa yuko kwenye mitandao ya kijamii anadhani ubunge ni mtandaoni, na hata hao mawaziri niliwaambia wawajibu wapinzani kwenye mitandao ya kijamii sikumaanisha wasije bungeni wanatakiwa pia wafike bungeni,” ameongeza Ndugai

Wiki iliyopita wakati wa Mkutano 13 wa Bunge Spika Job Ndugai aliwataja orodha ya wabunge na Mawaziri ambao ni watoro bungeni akiwemo Waziri Januari Makamba, Palamagamba Kabudi, na kwa wabunge alimtaja Godbless Lema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad