NEC Yafafanua Wabunge CHADEMA Kupita Bila Kupingwa

NEC Yafafanua Wabunge CHADEMA Kupita Bila Kupingwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imefafanua sababu za waliokuwa wabunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kupitia majimbo ya Babati Mjini, Ukerewe, Simanjiro, na Serengeti ambao baadaye walihamia CCM na walishinda kwenye nafasi hizo bila kupingwa.

Wabunge hao ambao walikuwa upinzani hasa CHADEMA ni aliyekuwa Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul, Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya, Joseph Mkundi wa Ukerewe pamoja na Marwa Chacha wa Serengeti.

Akizungumza  Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Giveness Aswile amesema kuwa,  wagombea  hao wanatoka katika vyama sita vya siasa ambavyo ni AFP, CCM, CUF, NCCR Mageuzi, NRA na UDP.

“Walitangazwa kuwa wamepita bila kupingwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi fomu za uteuzi, kukosa sifa kwa sababu mbalimbali zikiwemo kutorudisha fomu kwa wakati na wengine kutojaza fomu hizo kikamilifu.”

Aidha NEC imesema imezuia wagombea udiwani 29 ambao hawakuteuliwa kuwa kwa kushindwa kurejesha fomu za uteuzi, kutojaza fomu za uteuzi kwa usahihi, kutosaini fomu za kuheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi na kukosa sifa za kugombea udiwani kwa mujibu wa sheria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad