Nondo ataja sababu kuonekana mpinzani wa serikali

Nondo ataja sababu kuonekana mpinzani wa serikali
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Mtandao Wanafunzi (TSNP) Abdul Nondo amedai kuna kasoro kubwa ya mfumo wa elimu ndiyo sababu inayomfanya yeye binafsi na taasisi aliyokuwa akiiongoza kujihusisha zaidi na masuala ya kisiasa na sio masuala ya kitaalamu.

Akizungumza kwenye kipindi cha Eastafrica Breakfast, Abdul Nondo amesema hayo wakati akichangia mada changamoto za wanafunzi wa vyuo vikuu kushindwa kuwa washindani kwenye soko la ajira ambapo alitolea mfano wa vyuo vya ufundi.

“Tukitatua mifumo ya elimu yetu, hapa nchini hasa kuanzia kwenye taasisi za vyuo vikuu nchini na wakiacha vitu vinavyovumbuliwa na wanafunzi visitumike kwenye maonesho tu bali wawasaidie wanafunzi kuondoka navyo ili waende kujitangaza zaidi.” amesema Nondo.

"Mfumo wetu wa elimu lazima uende mbali zaidi na utafiti pia twende zaidi kwenye ugunduzi na ubunifu kwa kuwapatia mafunzo ya vitendo vya kutosha ili wanafunzi waweze kuwa washindana kwenye soko la ajira.” ameongeza.

Januari 5 mwaka huu Mahakama ya Hakimu mkazi Iringa ilimuachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia dhidi ya makosa ya aliyokuwa akishtakiwa ikiwemo kudaiwa kutekwa pamoja na kutoa taarifa za uongo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad