Mdau wa JamiiForums anasema amewahi kudhani kuwa fedha na sarafu za Tanzania zinatengenezwa kwa ubora wa kiwango duni na zinaachwa kwenye mzunguko kwa muda mrefu
Anasema kuwa Watanzania wanakunja noti bila ya mpangilio, noti zinahifadhiwa kwenye vifua(Wanawake) na wengi hawatumii 'pochi' kuhifadhi fedha
Kuna wafanyabiashara wanashika fedha huku wakiwa na mikono michafu mfano, wauza vimiminika kama mafuta, nyama, nafaka na Mkaa
Madhara ya uchafuzi huu ni makubwa kwani noti zinachakaa na kuilazimisha Serikali kuingia gharama za kuchapicha noti mpya
Mdau anaishauri Benki Kuu(BoT) ifanye mkakati wa kutoa elimu kwa umma juu ya njia bora ya kuhifadhi fedha na sarafu