Nyota wa Filamu na Mashabiki Wake Duniani Wasifia Ustadi Wake

Nyota wa filamu na mashabiki wake duniani wasifia ustadi wake
Stan Lee, mwandishi mashuhuri wa Marekani na rais wa zamani wa kampuni ya vichekesho ya Marvel Comics amefariki dunia akiwa na miaka 95.

Mwaka 1961, Lee alibuni filamu nne bora za Marvel Comics, na kuzipatia majina maarufu ikiwemo Spider-Man NA The Incredible Hulk.

Mwandishi huyo mkongwe wa vitabu vya vichekesho alifariki katika kituo cha matibabu cha Cedars Sinai mjini Los Angeles, kwa mujibu wa wakili wa familia.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya burudani ya Pow inayomilikiwa na Lee! alimtaja kama "Baba wa mitindo ya pop" kwa kubuni "wahusika wanaofahamika kote duniani".

Mkurugenzi mkuu Shane Duffy alimkumbuka kama "mwanzilishi wa kweli ambaye hana mpinzani".

Mke wa Lee, Joan, alifariki mwaka 2017.

Akizungumza na mtandao wa TMZ unaoangazia habari za nyota mashuhuri, binti yake JC Lee alisema mbaba yake alikuwa ''mtu mashuhuri na mwenye heshima".

Serikali 'yakaza buti' mzozo wa korosho Tanzania
Aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba : "katika utendakazi wake alihisi kuwa na wajibu mkubwa kwa mashabiki wake."

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, miaka ya hivi karibuni Lee, amekuwa akiiugua mara kwa mara.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Stan Lee au Stan Lieberman alizaliwa mwaka 1922
Lee alifahamika kwa kutengeneza filamu ya maarufu alipokuwa na kampuni ya filamu ya Marvel, japo aliachana na kampuni hiyo mwaka 1972.

Siku ya Jumapili, ambayo siku ya kuwatambua mashujaa , ukurasa wake rasmi wa Facebook uliweka picha za Lee akiwa jeshini, na kuandika kwa utani kwamba alikuwa mtunzi wa michezo tangu wakati wa vya pili vya Dunia.

Ruka ujumbe wa Facebook wa Stan LeeMwisho wa ujumbe wa Facebook wa Stan Lee
Stan Lee ni nani?

Lee alizaliwa mwaka 1922. Wazazi wake walikuwa wahamiaji wa kiyahudi kutoka Romania.

Alianza kufanya kazi katika sehemu ya kampuni ya machapisho ambayo hatimaye itabadilika na kufahamika kuwa Marvel Comics - na baadaye kuwa mhariri wa wasanii akiwa na miaka 18.

Alianza kufanya kazi kwenye sehemu ya Jumuia ya Machapisho ya wakati - kampuni ambayo hatimaye ilibadilika kuwa Marvel Comics - na kuwa mhariri wa wasanii akiwa na umri wa miaka 18.

Sheria za Usafiri Kenya: Maelfu wakumbwa na changomoto za usafiri
Sasa nina uume mpya nina matumaini ya kupata mpenzi
Kwa miaka kadhaa Lee alijikita zaidi katika uandishi wahadithi za uhalifu, hadithi za kuogofya na masuala mengine ya kijamii ili kuwavutia wasomaji wadogo.

Alipotimiza miaka 40 aliachana na vichekesho lakini mke wake alimshauri kuuni wahusika ambao angelipenda wahusishwe nae

Mwaka 1961, Lee na mchoraji Jack Kirby waliungana kubuni wahusika wanne maarufu sana- wahusika hao walikua tabia binafsi na matatizo yaliyohusiana

Timely Publications ilibadilishwa jina kuwa Marvel na ni hapo safari ya vitabu vya kichekesho ilianza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad