Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amechukua hatua hiyo baada ya kubainika kuwa ofisi hizo ndio chimbuko la utapeli na ubadhilifu wa ardhi jijini
Leo Novemba 29 amesema jiji hilo halina ardhi, halipangi, halipimi na wala halimilikishi lakini bado hadi sasa wanaendelea kutoa ofa za ardhi zinazoisumbua Wizara yake
Amesema kwa sasa yeyote mwenye ofa yenye muhuri wa jiji la Dar hautatambulika na kuwataka wahusika kwenda Manispaa kuuliza utaratibu mwingine
Ameeleza wakishaingia kwenye mfumo wa kidigitali ofisi za mikoa za ardhi hazitatambulika tena na kuanzia sasa maombi ya ardhi yatatoka wilayani kwenda kwa Kamishna ardhi wa wilaya husika
Aidha, Wafanyakazi katika ofisi zilizofungwa wanapaswa kuripoti kwa Kamishna Ardhi wa Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine
Amesisitiza kuwa walionunua viwanja kwenye mradi wa viwanja 20000 Dar na hawajaweka uzio ikifika mwisho wa mwezi Desemba Serikali itavichukua bila fidia