P Diddy Azinguliwa juu ya Kifo cha Mzazi Mwenzie



Diddy akiwa na aliyekuwa mke wake, Kim Porter
Msanii mkongwe wa muziki nchini Marekani, Puff Daddy 'Diddy', amekosolewa na mashabiki wake baada ya kuweka picha ya kuchekesha katika ukurasa wake wa instagram, ikiwa ni siku chache tangu alipofiwa na mke wake, Kim Porter.

Mkongwe huyo alipakia picha katika ukurasa wake, ambayo inamuonesha mtu mweusi akiwa na kopo la kinywaji huku akiambatanisha maneno ya shukrani (thanks giving), yanayozungumzia kitendo hicho kama ni likizo fupi ya maumivu anayopitia kwenye kipindi cha maombolezo ya mama watoto wake.



Katika maneno yaliyoambatana na picha hiyo, Diddy ameandika, "Ni mapumziko mafupi kutoka kuwa na huzuni, ninawapenda sana".

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wake wameonekana kumtetea na kusema kuwa kila mwaadamu ana jinsi yake ya kuomboleza.

Kim Porter alifariki November 15 na anatarajiwa kuzikwa Novemba 24, siku ya jumamosi nyumbani kwao Columbus, Georgia Marekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad