Polepole ataja viongozi watakaotemwa 2020

Polepole ataja viongozi watakaotemwa 2020
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema pamoja na ushindi ambao wanaoendelea kuupata kwenye chaguzi mbalimbali, lakini hawatakua tayari kuwarudisha viongozi mizigo kwa wananchi katika uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Polepole ametoa kauli hiyo leo Novemba 6, 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa mkoa na wilaya ya Kusini Unguja visiwani Zanzibar.

Polepole amesema wabunge na madiwani pamoja na wawakilishi wa CCM wanapaswa kujitathmini wakifahamu wana jukumu kubwa la kuwaletea maendeleo wananchi.

"Chama chetu hakikuwapa nafasi ya uongozo kama zawadi ili mwende mkale bata, tumewapa nafasi ya kuwatetea wananchi wenu na kutetea ilani ya chama chetu", amesema Polepole.

Polepole ameongeza kuwa, "Haiwezekani kuona wana CCM wanafanya kazi halafu kuna watendaji mnashindwa kuwajibika ipasavyo, mnapofanya vibaya lawama kubwa inakuja kwenye chama ambacho ndiyo chenye kutekeleza ilani yake".

Mapema mwezi Oktoba,  Polepole katika mahojiano yake na www.eatv.tv, alisema kuwa chama chake kiko katika mikakati ya kufanya mageuzi ya kiuongozi, kitaasisi na utendaji ili kukiimarisha zaidi.

"Tunafanya mageuzi ya CCM, katika nyanja za maendeleo kwakuwa chama ni taasisi, tutafanya mageuzi ya kiuongozi tutaeleza ni viongozi wa namna gani tunaowataka", amesema Polepole.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad