Polisi Yafunguka Kuhusu Waasi Kuingia Nchini

Polisi Yafunguka Kuhusu Waasi Kuingia Nchini
Baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa baadhi ya vijiji vilivyopo upande wa nchi ya Msumbuji karibu na mpaka wa Tanzania kuwa vimeshambuliwa na waasi, ikidaiwa huenda wameingia nchini Tanzania, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amesema hali ya mipaka iko salama.

Taarifa hizo zilisambaa leo, Novemba 26, 2018, na kupelekea www.eatv.tv kumtafuta Kamanda wa Polisi kutaka kujua undani zaidi wa jambo hilo na hali ya usalama ambapo amekanusha kuwa hakuna waasi wala wananchi wa msumbiji waliovuka mpaka na kuingia nchini kwasababu ya kushambuliwa.

''Mipaka yetu ipo salama, hakuna watu wala waasi walioingia nchini, askari wetu wapo kazini saa 24 hivyo wananchi waondoe hofu usalama upo wa kutosha na hakuna tukio kama hilo'', amesema Kamanda Mkondya.

Aidha Kamanda Mkondya amesema kuwa eneo la mpaka ni kubwa haliwezi kuwa na askari muda wote hivyo ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa endapo wataona watu wageni wasiowafahamu wameingia katika eneo lao.

''Wananchi tumeshawapa namba zetu za simu wakimuona mtu ambaye wanamtilia shaka wawasiliane na sisi haraka ili askari wafike katika eneo hilo mara moja, lakini kiujumla mkoa na mipaka yake viko salama''.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad