Producer S2kizzy kufuata nyayo za Nahreel na Luffa, Je Quick Rocka analipi la kusema?


Kama inavyofahamika studio ya SWitch Records  inamilikiwa na msanii Quick Rocka. Studio hii imeweza kutoa nyimbo nyingi kubwa kwenye Bongo Fleva ambazo zimefanya vizuri kwa kiasi kikubwa. 

Licha ya studio hiyo kufanya vziuri imekuwa na bahati mbaya kutokana na ma-producer wengi kutodumu hapo. Hufanya vizuri zaidi baada ya muda kidogo huondoka na kwenda sehemu nyingine. 

Kwa sasa Producer S2kizzy ameweka wazi kuwa ameshaondoka Switch Records na kwenda kufungua studio yake.S2kizzy ameandoka Switch Records baada ya kuweza kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Joh Makini, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Nikki wa Pili, Rayvanny, Rich Mavoko na wengineo kibao. 

S2kizzy sio wa kwanza 

Kabla ya S2kizzy kuanza kudondosha ngoma zake Switch Records alipokea kijiti hicho kutoka kwa Luffa ambaye alitimukia studio za Wanene Entertainmet. 

Luffa aliweza kujenga vilivyo kundi la OMG Tanzania ndani ya studio hiyo, ni kipindi ambacho kundi hilo lilikuwa lebo chini 

Switch Music Group (SMG). Pia Luffa aliweza kufanya kazi na wasanii kama Joh Makini, G Nako, Vanessa Mdee na wengineo. 

Hata hivyo kabla ya Luffa alikuwepo producer Nahreel ambaye pia ni msanii wa kundi la Navy Kenzo. Nahreel naye pia aliondoka na kwenda kufungua studio yake 'The Industry' iliyompa mafanikio makubwa hadi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards kama producer bora. 

Je, kuondoka kwa ma-producer ndani ya Switch Records pindi wanapokuwa kwenye kiwango cha juu kabisa cha mafanikio ni nani wa kunyooshewa kidole?, ma-produre wenyewe au uongozi (Quick Rocka) wa stuio hiyo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad