Prof. Ndalichako: Bodi ya mikopo haitatoa hata senti kwa wanafunzi wadanganyifu


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu haitaruhusu kwa mwanafunzi yoyote kupata mkopo kwa njia ya udanganyifu na kuwafanya wengine kukosa fursa hiyo. 

Prof. Ndalichako ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar, Riziki PembeJuma mjini Unguja. 

"Na wengine ambao wanachukua mkopo hata kimsingi ni ile ubinafsi lakini hawakuwa na uhitaji hizo fedha wangewaachia watoto ambao hawana uwezo kiukweli kweli, kuna watu wengine mpaka wanadanganya  wengine walikuwa wanajipa hata uyatima mpaka siku hizi inabidi tuwe tunafuatilia vyetu mtu akisema Yatima tujiridhishe," alisema Ndalichako. 

"Lakini watu walikuwa wanafika mahali wanadanganya ili wapate mikopo kwahiyo mimi niombe tu tuwe na uzalendo, tuangalie mikopo tumeweka kwa walio na uhitaji kwahiyo wewe kama huna uhitaji sio lazima wala huna sababu ya kwenda kuchukua tuachie watoto ambao bila huo mkopo hawawezi kusoma kabisa."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad