Rais Magufuli Hataki Kuona Wananchi Wakilipa Nauli- Waziri Majaliwa

Rais Magufuli Hataki Kuona Wananchi Wakilipa Nauli- Waziri Majaliwq
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Magufuli hataki kuona wananchi wakilipa nauli kwenda kufuata huduma za matibabu au kutembea umbali mrefu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akitembelea miradi ya Afya katika kituo cha afya cha Nkowe na kukagua ujenzi wa gereza la Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari magereza wa gereza hilo.

Majaliwa amesema kwa sasa wananchi hao hawana sababu ya kulipa nauli kwenda Ruangwa kufuata huduma za vipimo na matibabu katika hospitali ya wilaya kwani baadhi ya huduma hizo kama upasuaji, maabara, mama na mtoto zinapatikana katika kituo hicho.

“Rais John Magufuli anataka kila Mtanzania apate huduma za afya karibu na makazi yake ili asilipe nauli au kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya,” amesema Majaliwa.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa  na Bibi Asia Abdallh (kushoto) wakati alipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo hicho.

Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Paul Mbinga amesema kituo hicho kinahudumia wakazi 5,264 wa Kata ya Nkowe, Chienjele, Nandagala, Likunja na Mnacho.

Dkt. Mbinga amesema mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya uliogharimu shilingi milioni 500, umepunguza gharama kama kwenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya ambayo ipo umbali wa kilomita 20.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad