Rais Magufuli "Kuongoza Nchi ni Kazi Ngumu Sana"



Rais John Magufuli amesema hakuna kipindi anachopitia changamoto katika uongozi kama ilivyo sasa.

Amesema kuongoza nchi ni kazi ngumu na wakati mwingine anashindwa kulala kutokana na kukabiliwa na mambo mengi ya kufanya.

Ametoa kauli hiyo leo mchana Alhamisi Novemba Mosi, 2018 katika kongamano la uchumi na siasa lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

“Uongozi ni kazi ngumu sikutegemea ingekuwa ngumu hivi. Yaani ukiingia chumbani kwangu mafaili yamejaa hadi kitandani na kila moja lina umuhimu huwezi kulipeka kwa mtu mwingine,” amesema.

Pia, amezungumzia jinsi anavyopenda kuzungumza lugha ya Kiswahili akibainisha kuwa ndio lugha inayowaunganisha Watanzania.

“Nasikia watu wanasema hajui Kiingereza nimekuwa waziri nikasafiri nchi nyingi kwenye vikao huko nilikuwa napewa uongozi wakati mwingine wa mikutano mikubwa sasa nilikuwa nazungumzaje kama sijui, “ amesema.

“Ukiniambia kusafiri sijui wapi sijafika, nimetembea karibu dunia yote kwa sasa sina haja kwangu ni Utanzania kwanza na kipaumbele changu ni kuwatumikia Watanzania.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad