Rais Magufuli: Nilifunga Ndoa Bila Koti la Suti, Mke Wangu Bila Gauni la Bi Harusi nilikunywa Pepsi ye Alikunywa Milinda

Rais Magufuli: Nilifunga Ndoa Bila Koti la Suti, Mke Wangu Bila Gauni la Bi Harusi nilikunywa Pepsi ye Alikunywa Milinda
Rais wa Tanzania John Magufuli leo amesema alifunga ndoa bila kuvaa koti la suti na mkewe Janeth hakuvaa gauni la bibi harusi.

Ndoa hiyo ilifungwa wakati Magufuli akiwa mwanafunzi katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na haikuambatana na sherehe yoyote.

Akiongea leo katika mdahalo uliofanyika UDSM kutathmini miaka mitatu ya uongozi wake wan chi, Magufuli amesema amefurahi kurudi chuoni hapo ambapo si tu alipata elimu yake ya juu bali kufunga pingu za maisha.

"Siku niliyooa watu wengi hawakujua…na haimaanishi sikuwa na pesa ya kununua koti au gauni la harusi kwa mke wangu, sikuona kama vitu hivyo ni vya msingi sana."

"Tulienda hapo kanisani pete tukanunuliwa na Padre, tena zilikuwa za shaba. Padre pia alitununulia soda, nakumbuka mimi nilikunya pepsi na mke wangu alikunya mirinda...Baada ya hapo nikaendelea na shughuli zangu."

Padre ambaye aliwafungisha ndoa hiyo na kutoa ufadhili wa pete na soda kwamujibu wa Rais Magufuli anaitwa Msemwa na sasa yupo Tanga. "Mfuateni father (Padre) Msemwa yeye atawaeleza vizuri zaid."

Magufuli pia amesema hata ndoa za watoto zake haziambatani na sherehe kubwa, "mpaka sasa watoto zangu watatu wameshafunga ndoa na sikufanya sherehe kubwa. Mmoja alifunga ndoa tayari nikiwa madarakani lakini wala hamkusikia."

Novemba 2016 mke wa Rais Magufuli aliugua na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Hatua hiyo iliwashangaza wengi ambao walitarajia labda angepelekwa nje ya nchi kama ilivyokuwa ada ya vigogo pale walipofikwa na maradhi.

Toka alipoingia madarakani miaka mitatu iliyopita Rais Magufuli amekuwa mashuhuri ndani na nje ya Tanzania kwa hatua zake za kubana matumizi yasiyo ya lazima. Tukio hilo la harusi, ambalo ni la maisha yake binafsi linatoa mwangaza wakuelewa ni kwa nii Magufuli hatetereki katika kubana matumizi ya serikali yake.

Mwezi mmoja toka alipoingia madarakani alifuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania kwa mwaka 2015 na kuagiziza mabilioni ya fedha yaliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe hizo kutumika kujenga kipande cha barabara moja iliyokuwa sugu kwa foleni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya hatua kali alizozichukua katika kupunguza matumizi ya serkali ni kuratibu safari za nje za watumishi ambapo kwa sasa lazima mtumishi apate kibali ndipo asafiri nje. Hata yeye mwenyewe bado hajasafiri kutoka nje ya Afrika.

Yeye mwenyewe ametembelea nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia tu, tangu alipoingia madarakani.

Posho za vikao vya watumishi zimepunguzwa na nyengine kuondolewa kabisa, huku kumbi za mikutano zikitakiwa kuwa ni za serikali tu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad