Rais Museveni aitaka Uganda ‘The Cranes’ waifunge Taifa Stars,

Rais Museveni aitaka Uganda ‘The Cranes’ waifunge Taifa Stars,
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa licha ya timu yake ya taifa maarufu kwa jina la ‘The Cranes’ kufuzu kushiriki michuano ya Afcon hapo mwakani lakini lazima ihakikishe inapata ushindi kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania.



Museveni ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa  kijamii wa Twitter, ”Hata kama ‘the Cranes’ tayari mmeshafuzu, nafahamu kwamba bado mna mchezo mmoja wa kucheza dhidi ya Tanzania. Tafadhali hakikisha hampotezi kwenye mchezo huo. Pongezi kwa mara nyingine,” amesema Museveni.

Mara baada ya ujumbe huo wa Museveni, naye mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akaandika ujumbe wa kumtaka Rais huyo kuwa na ubinadamu kwakuwa timu yao tayari imeshafuzu.

”Mzee acha roho mbaya. Mmeshasahau mafuta yenu yanapita Tanzania? Shauri yako,” ameandika Zitto Kabwe.

View image on Twitter
View image on Twitter

Yoweri K Museveni

@KagutaMuseveni
 Even if the Cranes have already qualified, I know that they still have a game to play against Tanzania. Please make sure you do not lose that game. Congratulations once again.

659
10:14 AM - Nov 20, 2018
304 people are talking about this
Twitter Ads info and privacy

Yoweri K Museveni

@KagutaMuseveni
 · 2h
 Even if the Cranes have already qualified, I know that they still have a game to play against Tanzania. Please make sure you do not lose that game. Congratulations once again.


Katika mechi yake ya kwanza timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ alifanikiwa kutoka sare tasa ya bila kufungana 0 – 0 dhidi ya Uganda maarufu kama ‘The Cranes’ ambao walikuwa nyumbani.

Stars iliyopo kundi ‘L’ chini ya Mnigeria huyo ilijikuta ikipata kipigo cha mabao  3 – 0 mbele ya Cape Verde ugenini. Kisha kupata ushindi wa 2 – 0 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Cape Verde jijini Dar es Salaam.

Ikapoteza na Lesotho  kwa bao 1 – 0 mchezo uliyopigwa wikiendi hii iliyopita siku ya Jumapili.

Msimamo wa kundi hilo Uganda inaongoza kwa kuwa na pointi 13, Taifa Stars alama tano, Lesotho alama tano, na Cape Verde alama nne.

Kwa msimamo huo Uganda ishafuzu, ili Stars apate nafasi ya kwenda Afcon mwakani nchini Cameroon italazimika kuifunga Uganda mchezo wa marudiano Machi 22 uwanja wa Taifa, huku ikiomba Cape Verde  iifunge Lesotho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad